KUDADADADEK!!!!....PICHA 36 ZA KILICHOTOKEA KWA WEMA SEPETU JANA USIKU NA JINSI STAA WA NIGERIA OMOTOLA ALIVYOPOKEWA DAR.

Wema
Sepetu akizungumza muda mfupi baada ya watu kuchek sehemu ya movie yake
mpya aliyoizindua ya Super Star, ni movie yake ya kwanza na ndani kuna
mastaa kama T.I.D, Mr Blue, Barnaba, Hemed na wengine… baada ya hapa
Wema alitangaza safari ya kwenda kumpokea Omotola.

Wema
Sepetu na friends wakicheza ngoma iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi
ya Omotola Airport Dar es salaam, ilikua ni saa tisa na dakika ishirini
usiku.
Exclusive on millardayo.com
Meneja wa Wema Sepetu Martin Kadinda amesema kiwango cha pesa
kilichotumika kumleta Omotola Tanzania sio chini ya dola elfu saba za
kimarekani zaidi ya milioni kumi za kitanzania.
Amesema “mwanzoni tulikua
tunataka kumleta Genevieve Nnaj lakini alikua busy na ratiba,
tukamtafuta Ritha Dominic lakini gharama zake zilikua juu alikua anataka
dola elfu 23 za kimarekani, nikaona itakua ngumu kwetu kwa sababu
tunafanya wenyewe bila kuwa na udhamini baada ya kuhangaika ndio
tukampata Omotola.
Omotola atakuepo leo pale
Girrafe Ocean View kwa ajili ya family day, toka jana alitakiwa kuwa
kwenye uzinduzi wa movie lakini kutokana na kupata matatizo kwenye
ubalozi wa Tanzania Nigeria alichelewa ndege na kuingia Tanzania usiku
sana.






























