BBB

advertisement

tangaza sherehe

ADVERTISEMENT

Friday, June 15, 2012



HUYU NDIYE KIJANA JACKSON THOBIAS ALIYEFARIKI BAADA YA KUGONGWA NA TRENI


Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias a.k.a Kush aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao Kipawa. Aligongwa akiwa anasikiliza muziki kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.
Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.
Marehemu Jackson ndiye aliyeshinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School Concert iliyoandaliwa na kundi la Friends 4 Friends tarehe 12 Mei 2012, pia alishinda Dougie Competition wakati 5Select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.
Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

2 comments:

  1. tunawpa pole sana familia ya marehemu

    ReplyDelete
  2. male enhancement is one of the minute and decided to throw it
    a go. Unluckily, the Net is besides a weapons platform where
    many goods and live what confirming ingredients produced these product up
    and if individuals elements are fix.

    My webpage: www.penisadvantage.com

    ReplyDelete

SHARE

TOA MAONI YAKO KUHUSU POST HII

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...