HIVI ULISIKIA ILE STORI YA WACHEZAJI WA TWIGA STARS KUSHIRIKI MAPENZI YA JINSIA MOJA? KIPYA NDIO HIKI…HAPA

.
Vyombo mbalimbali vya habari 
vya Tanzania likiwemo gazeti la Mwananchi vimenukuliwa vikiripoti stori 
kwamba Kocha wa timu ya taifa ya Twiga Stars aliejiuzulu Boniface Mkwasa
 alisema moja kati ya mambo yaliyomkera Twiga Stars ni wachezaji kadhaa 
kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wao kwa wao kwenye timu.
Exclusive on millardayo.com 
Nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili amesema “nimefurahi kulizungumzia 
hilo swala kwa sababu limekua likizungumzwa kwenye magazeti mengi bila 
uthibitisho, kocha hakuzungumza kwamba kuna vitendo kama hivyo alisema 
vilikuepo kipindi cha nyumba lakini kwa sasa havipo, nimekua Twiga Stars
 toka 2006 mpaka sasa sijaviona hivyo vitendo labda mwalimu ndio aliona 
kwa mchezaji lakini hakuna yeyote ambae amewahi kuripoti kwangu”
“Wazazi wetu hawajapenda hili 
swala, tumedhalilishwa na hata kama kuna mchezaji alifukuzwa kutokana na
 hilo basi itakua ni siri kati yake na mwalimu hatujawahi kuambiwa, kama
 Mkwasa atapatikana ni vizuri amtaje huyo mtu il iwatanzania wajue 
lakini kiukweli hakuna vitendo kama hivyo Twiga Stars” – Sophia
Exclusive on millardayo.com leo
 Kocha Boniface Mkwasa amesema “sijafanya kikao chochote na waandishi wa
 habari kuzungumzia hilo swala na sijazungumza lolote kuhusu ishu ya 
usagaji nashangaa hawa waandishi wameipata wapi hii habari na wanazidi 
kujenga chuki, ndio maana nimekaa kimya wiki nzima sijaongea chochote, 
na sio kwamba nimetoka Twiga Stars ndio nikasema hayo, sijawahi 
kushuhudia hivyo vitu hata siku moja na kama vilikuwepo labda ni zamani 
sana kipindi bado hata sijaingia”
Kuhusu kuvipeleka Mahakamani 
vyombo vya habari vilivyoandika hizo habari, Mkwasa amesema “mimi 
sitafanya chochote namwachia Mwenyenzi Mungu tu kwa sababu kila mtu ana 
uhuru, ila waandishi wazitumie vizuri kalamu zao kwa sababu 
watasababisha wazazi wasiruhusu mabinti zao kuja kucheza kwenye timu ya 
taifa”
No comments:
Post a Comment