HATIMAYE WATU KWENDA ZANZIBAR KWA MAGARI YAO...!!!
Azam
yaamua kufanya kweli na hivi karibuni meli ya kisasa iko mbioni
kuzinduliwa ambayo ikawezesha watu kwenda na magari yao Zanzibar. Meli
hiyo inauwezo kubeba magari 200, abiria 1500 na Mizigo tani 500.
---
KAMPUNI ya
Usafiri wa baharini ya Azam Marine inatarajia kuzindua meli kubwa ya
kisasa kwaajili ya abiria waendao Dar es Salaam, Pemba na Unguja. Meneja
Mkuu wa kampuni hiyo Hussein Mohamed Said, amesema Julai 15 mwaka huu
meli hiyo yenye urefu wa mita 100 itazinduliwa.
Mohamedi
alisema shida ya usafiri itapungua kwa asilimia kubwa kutokana na meli
hiyo kuwa na uwezo wa kubeba abiria 1500, Mizigo tani 500 na magari 200
ambapo abiria atakae jisikia kwenda na gari lake Zanzibar, Pemba au Dar
es Salaam ataweza kufanya hivyo.Waziri
Mwenye dhamana ya Mawasiliano na Miundombinu wa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar Hamadi Masoud, alithibitisha kwamba anataaarifa za ujio wa
meli hiyo ambayo alisema kwa kiasi kikubwa itakuwa ni ya kutoa huduma tu
na siyakutengeneza faida.
Meli hiyo inauwezo wa kwenda kasi ya notkomail 20.
Nice! Nimeipenda hii
ReplyDeleteyaani jembe hunizidi mimi unajua zanzibar kuna uzi mpk leo usafiri wao mkubwa ni chai marage zile canter au vidaksan yaani daladala ni za kuhesabika
ReplyDeletenow ahaaa unabeba chako unavusha , cpatii picha wasanii wa bongo wakienda zanzibar kwenye tukio!aisee itakuwa mashindano ya gari za bei mbaya!!