ETHIOPIA YAAMISHA WATU ''KWA NGUVU''
Baadhi ya watu wanaohamishwa toka bonde la Omo |
Serikali ya Ethiopia imelaumiwa kwa kuwahamisha kwa nguvu maelfu ya watu kutoka mashamba yao ili kuacha
nafasi kwa upanzi wa miwa
Kwa muujibu wa shirika la Human
Rights Watch lililona makao yake mjini New York, uhamishaji huo wa watu
unafanyika katika bonde la Omo.
Bonde hilo ambalo limeorodheshwa kama sehemu ya
kuhifadhiwa duniani ,pia ndipo mahali bwawa kubwa limepangwa kujengwa.
Ujenzi wa bwawa hilo tayari limezua utata.
Lakini serikali ya Ethiopia imekanusha madai
hayo ya kuwahamisha watu kwa nguvu huku ikijitetea kwamba mradi huo
utazalisha nafasi zaidi za kazi.
Nalo shirika la Human Rights Watch limesema kuwa
maafisa wa usalama wanawahamisha watu kwa nguvu kutoka eneo hilo na
kuwalazimisha kurudi katika ardhi zao za kiasili.
Katika ripoti yao, shirika hilo limesema wakati
waliopkuwa wakizuru eneo hilo mwezi wa June 2011,walishuhudia makundi ya
kijeshi yakiwahangaisha na kutisha watu ili wahame na kutoa nafasi kwa
upanzi wa miwa. Katika harakati hizo wanajeshi wanadaiwa walikuwa
wakiiba na kuwauwa mifugo.
Hata hivyo serikali ya Ethiopia imekanusha madai hayo.
Msemaji wa serikali Bwana Bereket Simon amesema
palipokuwa na haja ya kuwahamisha watu , wahusika sote walishauriwa na
pia kushirikishwa.
No comments:
Post a Comment