Didier Drogba ahamia timu ya China
Aliyekuwa mshmabulizi matata wa Chelsea Didier Drogba amehamia klabu ya Shanghai Shenhua ya China.
Mwamba huyo ametia kandarasi ya miaka miwili-na-nusu na timu hiyo ya China.
Kujiunga na klabu hicho , kimemfanya awe timu moja na mchezaji mwengine wa Chelsea Nicolas Anelka.
Drogba mwenye umri wa miaka 34 amesema kabla ya kuamua kuhamia China alifikiria kwa makin sanai.
"Nilitilia maanani mialiko chungu nzima
niliopata katika kipindi cha wiki chache zilizopita , lakini nafikiri
kwa wakati huu kuhamia timu ya Shanghai Shenhua ulikuwa uamuzi mzuri"
Mwamba huyo wa Ivory Coast atakumbukwa kwa bao
alilofungia Chalsea walipocheza na Bayern Munich ya Ujerumani.Bao hilo
liliifanya Chalsea ijiandikie historia ya kushinda kombe la Klabu bingwa
bara Ulaya.
Drogba alijiunga na Chalsea mwaka wa 2004 kutoka
Olympic Marseille ya Ufaransa kwa pauni million 24. Alikuwa baadhi ya
wachezaji wa kwanza kusajiliwa na Meneja Jose Mourinho alipojiunga na
Chalsea.
Akiwa Chalsea kwa kipindi cha miaka minane,
Drgoba aliisaidia klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu ya Uingereza
mara tatu na kombe la FA mara nne.
Mwamba huyo wa Ivory Coast anaondoka Chalsea
akiwa ameandikisha historia ya kuifungia timu hiyo jumla ya magoli 157
hivyo kuwa mchezaji nambari nne katika kwa ufungaji wa magoli katika
historia ya Chalsea.
Katika kujiunga kwake na timu hiyo ya Shanghai
Shenhua , Drogba anasema jukumu lake la kwanza ni kufanya soka ya China
itambulike
No comments:
Post a Comment