Taarifa kutoka Marekani
zinaeleza kuwa Wizara ya Ulinzi ya Marekani itaipatia Kenya ndege nane
ndogo zisizohitaji rubani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi kwa nchi
za Afrika Mashariki, ili kuzisaidia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu
wa Somalia, al-Shabaab.

Gazeti la Wall Street Journal la Marekani
limearifu kuwa Kenya itapata ndege hizo ambazo hazitakuwa na silaha,
lakini zinaweza kugundua maeneo yanayofaa kulengwa na ndege au majeshi
ya ardhini.
Gazeti hilo limesema ndege zisizokuwa na rubani
ni sehemu ya msaada wa Marekani, pamoja na malori, zana za mawasiliano,
na silaha kwa Burundi, Djibouti na Uganda.
No comments:
Post a Comment