Utafiti mpya uliofanywa sehemu
mbali mbali za dunia, kutaka kujua wapi watu wanaficha fedha zao
kukimbia kodi, umegundua kuwa dola kama trilioni 20, zimefichwa nchi za
ng'ambo, mbali ya macho ya maafisa wanaotoza kodi.

Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la
utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya
matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa.
Dola trilioni 21 ni sawa na pato la mwaka la Marekani nzima pamoja na Japani.
Tax Justice Network inafikiri fedha zilizofichwa ng'ambo zinaweza kuwa zaidi ya hizo.
Ripoti yao inaonesha jinsi matajiri wakubwa
wanavohamisha fedha na kuziweka kwenye nchi zinazoweka siri, kama
Uswiswi na Visiwa vya Cayman, kwa kupitia mabenki ya kibinafsi.
Ripoti piya inaeleza kuwa nchi zenye utajiri wa
mafuta, kama Urusi na Nigeria, ndio hasa kwenye mtindo wa fedha kutoweka
na kuvushwa, badala ya kuwekezwa nchini.
Utafiti huo unamaliza kwa kusema wanasiasa
sehemu mbalimbali za dunia, wanategemea kuwa fedha hata zikiwa kwa watu
wa juu, zitavuja hatimae na kuwafikia maskini - ripoti inasema hayo
hayatokei tena.
No comments:
Post a Comment