Pages

Thursday, July 26, 2012

Dar Talk"Sinta Akimbiwa na Marafiki Kisa "Mashauzi"




DEMU mwenye makuzi ndani ya tasnia ya filamu bongo Christine John ‘Sintah’ aka J LO wa Bongo, inadaiwa kuwa kwa sasa wenda akakosa kabisa marafiki kwani tabia yake ya kujiona na dharau ndiyo inasababisha wengi kumkibia. Chanzo kimoja cha habari kilichozungumza na mwandishi wa DarTalk ambaye hakutaka jina lake litajwe, alidai kuwa msanii huyo amekuwa na urafiki na watu maarufu huku akisahau kuwa hao wanaweza kumkimbia muda wowote endapo akiishiwa. Chanzo hicho kilisema kuwa wiki iliyopita alitofautiana na mmoja kati marafiki zake wakubwa na hali hiyo ndiyo inayosababisha hata wale wengine kuhisi kuwa mwanadada huyo ni mtu asiye na upendo kwa wengine kutokana na tabia yake ya kujiona. “Wiki iliyopita tu katofautiana na msanii mwenzake naweza kumtaja jina lakini itakuwa si vizuri, hivyo yupo katika wakati mgumu kwani ana majivuno mno na kuna time anakera sana kwa tabia zake za kujiona yuko juu zaidi ya wengine,” Kilidai chanzo hicho. Katika harakati za kumtafuta Sintah ili aweze kujibu mapingo ya kutofautiana na mwenzake na kukimbiwa na marafiki, alijibu kuwa hiyo haimuhusu mtu kwani anaishi maisha yake na hana bifu na mtu hivyo haoni kama kuna mtu anaweza kumtisha kwa lolote. “Huyo aliyekupa hizi taarifa ungemwambia akutajie na jina la huyo msanii nilitofautiana naye, sasa kwanini unaniuliza mimi, kwanza suala la mimi kukimbiwa na marafiki yeye linamuhusu nini kama si matatizo aliyonayo,” alijibu. Pia demu huyo aliongeza kuwa kwa upande wake hana urafiki na watu au wasanii wale wasiojishungulisha na kazi ama biashara nyingine nje ya filamu.

No comments:

Post a Comment