JESHI LA MISRI LAJILIMBIKIZIA MADARAKA
Baraza la kijeshi linalotawala 
limetangaza amri ya kijilimbikizia madaraka huku nchi hiyo ikisuibiri 
matokeo ya uchaguzi wa urais.
Mwenyekiti wa baraza la kijeshi  ,Hussein Tantawi.....Stakatadhi kutoka kwa baraza kuu la kijeshi linasema kuwa uchaguzi mkuu mpya hauwezi kuandaliwa hadi kuwe na katiba mpya.
Kutokana na amri hiyo, sasa baraza hilo la kijeshi linachukuwa mamlaka ya mbunge.
Wakati huo huo chama cha Muslim Brotherhood 
kimetangaza kuwa mgombezi wake Mohammed Mursi, ndie mshindi wa uchaguzi 
wa urais uliofanywa siku ya jumapili.
Bwana Mursi, anashindana na Ahmed Shafiq, ambaye alikuwa waziri mkuu wa mwisho katika serikali ya Hosni Mubarak.
Chama hicho cha Muslim Brotherhood kimesema 
kwamba baada ya kura zote kuhesabiwa mgombezi wao anashikilia uongozi wa
 kati ya 52%-48% dhidi ya Bwana Shafiq.
Kituo cha Televisheni kinachounga mkono chama 
cha Muslim Brotherhood kimetangaza kuwa Bwana Mursi amepokea kura zaidi 
ya milioni 13. Nacho kituo cha televisheni cha kitaifa kimetangaza 
kwamba anaongoza katika kura hizo.
Akihutubu katika makao makuu ya chama chao ,Bwana Mursi ameahidi kuwa atakuwa rais wa Wa-misri wote na kwamba hatalipiza kisasi.
Lakini wasimamizi wa kampeni za Bwana Shafiq 
wamepuuza tangazo linalodai kuwa Bwana Mursi ndie mshindi wa uchaguzi wa
 siku ya jumapili.

No comments:
Post a Comment