GARI LA MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE ''RAY'' LAWAKA MOTO USIKU
GARI
 la msanii maarufu wa filamu hapa nchini, Vincent Kigosi ‘Ray’, juzikati
 liliwaka moto usiku na kuteketea katika Viwanja vya Leaders vilivyopo 
Kinondoni jijini Dar.
 Kikiongea na Ijumaa Wikienda, chanzo chetu 
makini ambacho kilikuwa jirani na eneo la tukio wakati gari hilo 
linaungua, kilisema kuwa wakiwa wanasikiliza muziki uliokuwa ukipigwa 
katika gari hilo kwa mbali, walishtuka kuliona linafuka moshi eneo la 
mbele, majira ya saa tano usiku.

 
“Kiukweli tulishtuka sana kuona 
gari la Ray likiwaka moto bila kujua nini chanzo… mpaka tunafika sehemu 
gari hilo lilipokuwa limeegeshwa, tulikuta tayari kila kitu kimeungua,” 
kilisema chanzo hicho ambacho ni msanii wa filamu.
 Ray alipotafutwa 
kwa njia ya simu, alikiri kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa baadaye
 gari hilo lilikokotwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay na
 baada ya uchunguzi kukamilika, lilipelekwa gereji tayari kwa 
matengenezo.
 “Kweli ajali ilitokea pale Leaders Club na kusababisha 
kila kitu kilichokuwa ndani ya gari kuteketea. Lilipelekwa Oysterbay 
Polisi kwa ajili ya uchunguzi na ulipokamilika lilipelekwa gereji ya 
Wachina ya Sinza kwa matengenezo zaidi ingawa kwa hali liliyonalo sijui 
kama litatengenezeka.
 “Nasubiri majibu kutoka TRA, kama wataweza 
kuligharamia matengenezo itakuwa sawa lakini ikishindikana basi itabidi 
nilipwe gari jipya kwani lilikuwa na bima kama ilivyo sheria ya TRA 
kwenye ajali kama hizi,” alisema Ray.
SOMEWHERE BLOG  inakupa pole sana jembe, shukuru mungu wewe umepona inshaalah!...... 
 
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment