Pages

Thursday, July 12, 2012

Rose: Sirudi kwa Chuz ng’o


 Rose Michael 
KUFUATIA uchumba wa Mkurugenzi wa Chuz Entertainment, Tuesday Kihangala ‘Chuz’ na Rose Michael kuvunjika, demu huyo amefyatuka akidai kuwa katu hawezi kurudi kwa staa huyo.
Akipiga domo na paparazi wetu juzi jijini Dar, Rose alisema alikuwa akivumilia mateso nyumbani kwa mwanaume huyo akiweka ‘plaini’ kwamba kila mara migogoro ilikuwa haiishi ndani hivyo hata kikitokea kipya gani hawezi kurudi.
“Kwa sasa niko nyumbani namuomba Mungu anipe mwanaume ambaye ndiye riziki yangu, lakini ofisini (kwa Chuz) nakwenda kama kawa kwani atabaki kuwa bosi wangu,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment