Taarifa kutoka Nigeria zinasema
watu kama kumi wamekufa kwenye moto uliotokea kwenye meli iliyobeba
mafuta, kwenye bandari ya Port Harcourt.

Inaarifiwa moto huo ulisababishwa na cheche za moto kutoka ukarabati uliokuwa ukifanywa.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema baadhi ya
watu waliorushwa majini na mripuko huo, walinusurika, lakini wengi
wengine walinasa ndani wa meli.
Inadaiwa wazima moto hawakuweza kufikia meli hiyo, kwa sababu mipira ya maji ilikuwa mifupi.
No comments:
Post a Comment