
BAADA ya kuripotiwa kwamba Bosi wa Kundi la Fukuto Art Promotion la jijini Dar, Tuesday Kihangala ‘Mr. Chuz’ (pichani) ametapeli fedha shilingi milioni 500,000 imevuja kuwa aliyetapeliwa ni ndugu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),Joseph Kabila, aitwaye Itien Kabila.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Kabila ambaye ni mfanyabiashara kati ya Congo na Tanzania alimkopesha fedha hizo Mr. Chuz kwa ajili ya makubaliano ya kufungua kampuni ya kusambaza filamu jijini Dar.
Hata hivyo, mpaka sasa Mr. Chuz hajatimiza lengo hilo na amekuwa akikwepa kukutana na kupokea simu za Kabila.
Kabila amepanga kuzuia filamu ya Mr. Chuz ya ‘Dirty Game’ inatarajiwa kuingia mitaani hivi karibuni ili kufidia fedha zake.
Mwandishi wetu alipompigia simu, Mr. Chuz kuhusiana na sakata hilo alisema kuwa yeye anafanyabiashara na jamaa huyo na wala hajamtapeli.
“Miye sijamtapeli ingawaje ni kweli kuwa tarehe za kumrudishia fedha zake zimepita ila nilimtumia ujumbe kwenye simu yake kumfahamisha hali halisi,” alisema Chuz.
Hata hivyo, Kabila amesema hajapokea ujumbe wowote kutoka kwa Chuz.
No comments:
Post a Comment