Fernando Alonso ameshinda
mashindano ya mbio za magari ya Grand Prix ya Ujerumaini kwa Ferrari
yake siku ya Jumapili akiendelea kuongoza katika mbio hizo za Formula
One.
Bingwa mtetezi wa mara mbili mfululizo wa
mashindano hayo Sebastian Vettel wa timu ya Red Bull, kwa mara nyingine
ameshindwa kupata ushindi nyumbani kwake, lakini alimpita Jenson Button
wa McLaren ukisalia mzunguko mmoja katika mizunguko 67 kwa nafasi ya
pili.
Button
alisumbuliwa na matatizo ya matairi katika mizunguko michache ya mwisho
baada ya kumpatia changamoto Alonso katika kuongoza.
Alonso alikuwa dereva wa kwanza kushinda mbio tatu katika msimu huu.
Baada ya kusheherekia kwa kufungua champagne na
kuhojiwa jukwaani na bingwa wa mara tatu Niki Lauda Alonso alisema:
''Ilikuwa ngumu, si mashindano rahisi.
"Labda tulikuwa wepesi, lakini tulikuwa
washindani thabiti kuweza kuongoza pamoja na mpangilio mzuri kutoka
katika timu. "Baada ya kituo cha pili, nilipokabiliwa na ugumu, gari
lilikuwa katika hali nzuri na katika kasi ya juu kabisa kutawala
mashindano.''
Hata hivyo Vettel, alikuwa akimlalamikia
Hamilton alipojiweka pembeni ya mzunguko akisema: ''Sikuona umuhimu
wowote wa kufanya hivyo.
"Ilikuwa ni upuuzi kiasi fulani kukanganya
waliotangulia. Kama alitaka kuongeza kasi, angerudi nyuma na kutafuta
upenyo na kuongeza kasi tena. Kwa ujumla sifurahii kabisa''
Akimzungumzia uchunguzi wa Vettel kuhusu hatua
yake kuwapita ghafla wenzake, Button alisema: ''Hakuna cha kuzungumza.
Kamera za Televisheni zinaelezea kila kitu.
''Ni bora niongelee mashindano. Yalikuwa mazuri, niliyafurahia sana.''
''Ni bora niongelee mashindano. Yalikuwa mazuri, niliyafurahia sana.''
No comments:
Post a Comment