Pages

Saturday, July 21, 2012

Aliyefumania naye anaswa




Dakika chache baada ya habari ya mwanadada aliyewahi kuwa mwandani wa mwanamuziki Nice Lucas Mkenda ‘Mr Nice’, Lulu John kuingia mitaani akidai kumfumania mumewe Abdulatif Salum, jipya limeibuka, Risasi Jumamosi lina cha kukumegea.
Mara baada ya gazeti pacha la hili, Risasi Mchanganyiko, toleo namba 922 la Julai 18, mwaka huu kuruka na habari hiyo ukurasa wa mbele ikiwa na kichwa ‘USIOMBE YAKUKUTE’ ndipo akaibuka mwanamama aitwaye Rose mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, akidai kuwa gazeti hilo limemsaidia kumnasa ‘mwizi’ wa mali zake kwa mumewe.
Akizungumza na Risasi Jumamosi, Rose alisema kuwa mwanaume aliyefumaniwa na Lulu ni mumewe wa ndoa hivyo, ameapa kumsaka binti huyo popote ili amkomeshe aachane na mume wake.
“Tifu (Abdulatif) ni mume wangu wa ndoa. Huyo Lulu naye ni mwizi tu, namshangaa anadai kafumania wakati naye namsaka akione cha mtema kuni,” alisema mwanamama huyo na kuongeza:
“Nilishasikiasikia sana kuwa Lulu ananiibia mume wangu, nashukuru Risasi kwani niliposoma habari hiyo aya ya kwanza tu, nikajua ni kweli naibiwa.”
Alipoulizwa kuwa inaonekana anashahabikia kitendo cha mumewe kufumaniwa, Rose alisema: “Naye nimemuweka kiporo kwani amesafiri, akitia mguu nyumbani tu patachimbika wee ngoja uone.”
Risasi Jumamosi lilipomgeukia Lulu ili kumweka ‘mtukati’ juu ya kesi inayomkabili ya kutembea na mume wa mtu akitamba kuwa ni wake, simu yake iliita bila kupokelewa hata hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.

No comments:

Post a Comment